
Hatimaye mtendaji mkuu wa klabu ya Inter Milan, Beppe Marotta amethibitisha kuwa mshambuliaji wa klabu hiyo, Romelo Lukaku atarejea tena katika klabu ya Chelsea mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake wa mkopo kuisha.
–
Beppe amesema Lukaku bado hajawa kwenye kiwango ambacho walizoea kumuona miaka ya hapo nyuma
–
Lukaku ameanza kwenye kikosi cha kwanza katika mechi nane pekee katika klabu ya Inter Milan msimu huu akifunga magoli 5 na assist moja, muda mrefu akiuguza majeraha.