
Mkuu huyo wa wilaya ya Nachingwea alimuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Injinia Chionda Kawawa kuacha mara moja tabia ya kuwapangia majukumu mengine maafisa Kilimo wa wilaya hiyo.
Moyo alisema kuwa Wananchi wa wilaya ya Nachingwea wanatakiwa kupata elimu ya kilimo ili kuondokana na njaa ya mara kwa mara ambayo wamekuwa wanakumbana nayo.
Alisema kuwa ardhi ya Nachingwea inakubali kila aina ya zao hivyo hakuna haja ya wananchi kulalamika wanajaa wakati ardhi na nguvu wanazo za kutosha kufanya shughuli za kilimo na kujikomboa kiuchumi.
Moyo amewataka maafisa Kilimo kuacha tabia ya kukaimu nafasi ya mtendaji wa kijiji na kata kwa kuwa wanatakiwa wakatimize majukumu ya kutoa elimu ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa Wananchi wa Nachingwea wanautajiri wa kutosha kutoka kwenye ardhi yao iliyobarikiwa kuwa na rutuba ambayo inakubali kilimo cha mazao yoyote yale.
Moyo alimalizia kwa kuwataka maafisa Kilimo kuandaa ratiba maalumu ya kuwatembelea wakulima wa kila Kijiji kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo na ratiba hiyo apewe nakala ofisini kwake.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT