1 KULA CHAKULA CHA MTU USIEMJUA.
Acha kabisa uroho dunia sasa imebadilika sio kila unaemuona ana dhamira nzuri chips na kuku zitakuua.
–
2 KUKUBALI WITO WA MTU USIEMJUA.
Unapigiwa simu njoo sehemu fulani unakwenda na mtu humjui hii ni hatari sana. Mwambie yeye aje sio wewe umfate alipo.
–
3 KUPOKEA ZAWADI KWA MTU USIEMJUA.
Kuna watu ni machizi zawadi mtu humjui anakupa zawadi au hela unachukuwa. Kaa na shida yako hakuna kitu cha bure kwa dunia hii wa wandawazimu wengi kuliko wazima.
–
4 KUOMBA LIFTI KWA MTU USIEMJUA.
Acha hayo mambo utakwenda kufa kijinga kwa ushamba wako wa AC ya kwenye gari. Kama una haya ya baridi vunja mabarafu ya mia mia ujifunge kichwani.
–
5. KUAMINI WATU USIEWAJUA.
Yaani mtu hata humjui ulikutana nae tu kwenye nyumba ya ibada unamkaribisha kwako hii hatari. Sio jambo baya ila jipe muda watu wamebadilika hata wauaji nao tunaswali nao katika majumba ya ibada