Kocha wa klabu ya Kagera Sugar Mecky Maxime amekabidhiwa tuzo na zawadi ya kocha bora wa mwezi Februari, 2023 baada ya kuwa na mwezi mzuri akiiongoza Kagera Sugar kushinda mechi 2 na sare moja bila kupoteza mchezo.
ADVERTISEMENT
–
ADVERTISEMENT
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja kutoka Benki ya NBC Salama Mussa katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliomalizika kwa kichapo cha 2-0 kwa Wanankurukumbi ugenini dhidi ya KMC.