Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Anambra, nchini Nigeria, amemkamata Bw. Ikechukwu Obiora, kwa madai ya kumkaba mkewe aliyekuwa mjamzito hadi kufa katika eneo la Otolo Nnewi, Nnewi Kusini mwa jimbo hilo.
–
Imeripotiwa kwamba mshukiwa alimvamia na kumuua mkewe, Bi Ebere Obiora, mnamo Alhamisi, Machi 2, 2023 baada ya kuchelewa kumfungulia geti aingie ndani.
–
Akikiri kosa hilo, Ikechukwu aliripotiwa kuwaambia wakwe na mashemeji zake kwamba, “Nilirudi nyumbani asubuhi ya Machi 2, 2023, na nilikuwa nikigonga getini, lakini mke wangu hakufungua kwa haraka. Kwa hasira, nilianza kumfokea.
Kwanza nilimpiga kofi na kumpiga kuanzia getini mpaka ndani kabla ya kumshika shingoni kwa hasira na kumkaba hadi kufa. Sikuamini kilichotokea kwa sababu sikutarajia kwamba vitendo kama hivyo vingesababisha kifo chake. Hatimaye niliiacha ile maiti na kuondoka kwa woga na kuchanganyikiwa, baada ya kuwaeleza watu wachache ambao niliomba ushauri wa nini cha kufanya.