Mbunge wa bunge la seneti nchini Japan ametimuliwa kazini baada ya kutohudhuria kikao chochote cha bunge kwa mieza saba.
–
Mwanaume huyo ambaye ni maarufu sana katika mtandao wa You Tube – amekuwa mbunge wa kwanza kufutwa kazi bila kuwahi hata siku moja kuingia bungeni tangu achaguliwe
–
Maseneta walimfuta kazi Seneta Yoshikazu Higashitani Jumanne kwa kutohudhuria vikao vya bunge. Tangu achaguliwe miezi saba iloyopita, hajawahi kuhudhuria hata kikao kimoja cha bunge.
–
Mwezi Julai 2022, Bw Higashitani alichaguliwa kama seneta, Seneta huyo anayefahamika kwa jina maarufu kama ‘GaaSyy’ kwenye YouTube ambako ni maarufu sana kwa video zake maarufu – amekuwa ni senet awa kwanza kuwahi kufukuzwa kazini kwa kukataa kuhudhuria vikao.
–
Kufutwa kazi ndio adhabu kubwa zaidi ambayo mbunge anaweza kupewa nchini Japan. Taarifa zinasema kuwa mbunge huyo anaishi katika Milki za Kiarabu
–
Vyombo vya habari vya Japan vilisema kuwa alikataa kuhudhuria vikao vya bunge kwa hofu ya kukamatwa kwa shutuma za wizi na kumtusi mtu mashuhuri.