Mchungaji Eliona Kimaro arejea Kanisa la Ushirika la KKKT Kijitonyama, shangwe nderemo vyatawala wengine washindwa kujizuia waangua kilio.
Hiyo imejidhihirisha kupitia video iliyosambazwa usiku wa kuamkia leo ikimuonesha mchungaji huyo anawasili na kuwasalimu waumini, imekuwa baada ya kipindi fulani kukosekana machoni pa waumini wa kanisa hilo ambao walitokea kuvutiwa na kupendezwa na mafunzo pamoja na maubiri yake yaliobeba uzito uliogusa zaidi nyoyo zao.
Ikumbukwe kuwa Mchungaji Kimaro aliwahi pewa likizo ya muda wa siku 60 kutokana na sababu zilizomuhusisha katika ulinganifu wa imani ya umaminifu kati ya vijana wa dini ya Kiislamu na Wakikristo, hali ambayo ilizua sintofahamu kwa wanajamii wanaomzunguka na kuleta matokeo ya aina hiyo.