Kampeni ya kuchangisha fedha iliyoendeshwa na mchekeshaji wa Ethiopia, Eshetu Melese imefanikiwa kukusanya zaidi ya $1.6m (Bil. 3.7) ndani ya saa 48 kwa ajili ya uchangiaji wa ujenzi wa kinachotajwa kuwa kituo cha huduma za afya kwa watu wasio na makazi nchini humo.
–
Michango hiyo imetoka kwa wachangiaji ya 15,200 huku mchangiaji wa juu kabisa akitoa $10,000 (zaidi ya milioni 20).
–
“Saidia kubadilisha maisha ya idadi kubwa ya wazee na walio na changamoto ya akili wanaoishi katika hali mbaya ya maisha mitaani – tusaidie kuwajengea makazi” kinaeleza kiunganishi mtandaoni cha kampeni hiyo.
–
Mchekeshaji huyo pia amesaidia kupatikana kwa michango kutoka katika benki za nchini humo ingawa kiwangco kilichochangwa na benki hizo hakijawekwa wazi.