Shirika la usafirishaji kwa njia ya maji Lifeat Sea Cruises limefungua nafasi za kujihifadhi kwa safari zake za miaka mitatu kwenye meli ya MV Gemini, ambayo moja kwa moja itaanzia Istanbul mnamo Novemba 1 kuzunguka maeneo mbalimbali duniani.
–
Kampuni hiyo inaahidi kuweka alama kwa kufika kwenye bandari 375 kote duniani, ikitembelea nchi 135 na mabara yote saba.
–
Meli hiyo itasafiri zaidi ya maili 130,000 katika kipindi cha miaka mitatu, ikiwapitisha wasafiri wake kwenye vituo vya kuvutia kwenye kona mbalimbali za dunia vikiwemo visiwa pendwa mbalimbali vya kitalii ambapo kwa mwaka mmoja utalipia Dola za Marekani 30,000 sawa na Tsh Milioni 70 ambapo huduma zote muhimu utazipata humo ndani kama maisha ya kila siku tu unapokuwa kwenye maisha ya nchi kavu ya kila siku.