Nyota wa zamani wa Ujerumani, timu ya soka ya Real Madrid na Arsenal, Mesut Özil, ametangaza kustaafu soka la kulipwa. “Nataka kuwashukuru Shalke, Werder, Real Madrid, Arsenal, Fenerbahçe na Basaksehil, marafiki zangu wote katika soka, ilikuwa ni safari ya kustaajabisha” Ozil
Alistaafu katika kikosi cha taifa mwaka 2018 huku kukiwa na mjadala wa kisiasa nchini Ujerumani kuhusu wimbi la wahamiaji na wakimbizi na baada ya mzozo kuhusu picha iliyopigwa na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, akisema alikabiliwa na “ubaguzi wa rangi na kutoheshimiwa” juu ya babu yake wa Uturuki. “Ninatangaza kustaafu mara moja kutoka kwa soka ya kulipwa.
Nimekuwa na fursa ya kuwa mchezaji wa kulipwa kwa takriban miaka 17 sasa na ninahisi kushukuru sana kwa nafasi hiyo,” Ozil alisema katika taarifa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii Jumatano.
“Lakini katika wiki na miezi ya hivi karibuni, baada ya kupata majeraha, imekuwa wazi zaidi kuwa ni wakati wa kuondoka kwenye hatua kubwa ya soka.”