Baada ya mvutano wa muda mrefu uliohusisha wanandoa hawa wawili Dr Mwaka na Mkewe kwa kutoelewana kwa muda mrefu na hadi kufikia mwanamke kudai talaka kwa muda pia bila kupewa kwa wakati na kumuweka katika kigugumizi cha kushindwa kung’atuka kutoka mahusiano hayo, sasa matokeo yaja mapya.
Mkewe amedhihirisha kuwa ameondoka kwa mumewe ‘Dr Mwaka’ bila ya kupewa talaka aliyowahi kuipigania na kwenda kuishi mahala pengine pamoja na watoto.
Afunguka kufurahia kupata dili la Ubalozi ambalo pia linampa ujasiri wa kupambana na pia ameonesha nia ya kuomba apate madili mengi zaidi ya hilo.
Aidha ameongeza kwa kusema kwa sasa yupo Single japo hayupo tayari kuingia katika mahusiano mapya kwa sasa ingawa kuna watu wenye nia wanaweza jitokeza.
Credit; SnS&BONGO.5