Mesut Ozil amemtangaza kocha wa Roma, Jose Mourinho kuwa ndiye Kocha Bora wa soka kuwahi kutokea karne hii.
–
Ozil mwenye umri wa miaka 34, ambaye alitangaza kustaafu wiki hii, alichezea chini ya kocha Mourinho katika klabu ya Real Madrid ya Hispania.
–
Mourinho ndiye alimshawishi mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kusaini Real Madrid badala ya kwenda Barcelona kipindi hiko ambayo ilikuwa chini ya kocha Pep Guardiola.
–
Katika mahojiano yake na Marca, Ozil alieleza: “Kwangu mimi, Jose Mourinho ndiye kocha bora wa karne hii, uelewa wake wa kimbinu uko kwenye ngazi nyingine, lakini pia namna yake ya kuongea kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Kwa kweli yeye ni meneja wa kiwango cha ulimwengu”
–
“Nilimchagua Real kwa ajili yake alinipeleka kuona uwanja na vikombe vyote walivyoshinda, hiyo ilinifanya nipate ushawishi. Ziara ya Barcelona haikuwa na msisimko na kilichokatisha tamaa zaidi ni kwamba Pep Guardiola hakujisumbua kukutana nami” alisema Ozil
–
Ozil alijiunga na Real Madrid mwaka Agosti 17, 2010 akitokea klabu ya Werder Bremen ya Ujerumani, akiwa na miamba hiyo ya soka ya Hispania akicheza jumla ya mechi 159 akifunga mabao 27 na kutoa asisti 81.