Mkali wa muziki wa Amapiano nchini Afrika Kusini, Costa Tsobanoglou maaarufu Costa Titch kufariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Johannesburg.
–
Taarifa na vipande vya video kutoka vyanzo mbalimbali nchini humo zimeeleza kifo cha msanii huyo aliyekuwa na miaka 27 kimetokea baada ya kuanguka ghafla jukwaani kwenye tamasha la Ultra Music.
–
Costa Titch aliyetamba na ngoma kali Afrika ikiwemo Big Flexa ulotazamwa zaidi ya mara milioni 45 inadaiwa alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.
–
Enzi za uhai wake alifanya kolabo na wasanii wa Tanzania akiwemo Diamond Platnumz, Mbosso huku akiwa kama densa kwenye wimbo wa Ommy Dimpoz Wanjera.
–
Kifo hicho kimetokea ikiwa ni mwezi mmoja tangu nchi hiyo imempoteza rapa AKA aliyefariki dunia Februari 10.