Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameweka wazi nia yake ya kugombea Urais wa Taifa hilo katika uchaguzi mkuu nchini humo utakaofanyika mwaka 2026.
ADVERTISEMENT
–
Jenerali Muhoozi, kupitia ukurasa wake wa Twitter ameweka ujumbe huo huku akidhihirisha kwamba ni majibu kwa wale waliokuwwa wakihoji suala la yeye kugombea Urais.
ADVERTISEMENT
–
“Mmenitaka mimi kulisema daima! Sawa, kwa jina la Yesu Mungu wangu, kwa jina la vijana wote wa Uganda na dunia na kwa jina la mageuzi bora, nitagombea Urais mwaka 2026!” Ulisomeka ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter.