Kutoka nchini Kenya Mwanaume mmoja amejinyonga na kufariki dunia ukweni kwake baada ya jitihada za kumbembeleza mkewe kurudi nyumbani kugonga mwamba.
–
Inaelezwa kuwa mwanaume huyo ambaye jina lake bado halijafahamika alikwenda ukweni kwake Kijiji cha Kolondo Mashariki mwa Homa Bay, lengo likiwa kumrudisha mke wake aliyekuwa amerudi nyumbani kwa wazazi wake baada ya migogoro ya kifamilia.
–
Inadaiwa kuwa hapo awali, mwanaume huyo aliondoka na kwenda kusikojulikana, lakini baadaye alirejea usiku kimyakimya nyumbani hapo na kuchukua uamuzi wa kujinyonga.
–
Chifu wa eneo hilo, Perez Okoth amethibitisha kutokea tukio hilo, akisema mwili wa mwanaume huyo ulikutwa ukining’inia kwenye mti ulioko karibu na nyumba ya mama mkwe wake Jumapili,
Machi 12 asubuhi.