Kulingana na ripoti mwanafunzi wa Mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Maseno auawa kwa kupigwa risasi jana Jumatatu na polisi wakati wa maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali eneo la Kisumu huko nchini Kenya.
–
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi kuhusu tukio hilo, marehemu; William Mayange, alikuwa miongoni mwa kundi la wanafunzi waliojiunga na maandamano ya Azimio ambayo baadaye yaligeuka kuwa ya vurugu baada ya waandamanaji hao kuvamia duka kubwa lililopo eneo la Maseno.
–
Mwanafunzi huyo alijeruhiwa shingoni na kutangazwa kufariki alipofika katika hospitali ya Coptic ambako alikuwa amekimbizwa kupata matibabu.
–
Polisi wanasema wanafunzi hao waliwazidi nguvu maafisa wa usalama waliokuwa wameishiwa na vitoa machozi.
–
Source: Citizen Digital