Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamimi ya Chadema, Sylvester Masinde amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa anapatiwa matibabu.
ADVERTISEMENT
–
Taarifa iliyotolewa leo Machi 15, 2023 na Chadema na kusainiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mrema imeeleza Masinde amefariki dunia leo saa 11:25.
–
ADVERTISEMENT
“Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, wajumbe wa bodi ya udhamini, marafiki, viongozi na wanachama wa Chadema kwa msiba huu,” imeeleza taarifa hiyo.