ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, December 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

MWENYEKITI WA CHAMA CHA  MABENKI TANZANIA (TBA) AONGOZA MAADHIMISHO  SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SEKTA YA MABENKI.

I am Krantz by I am Krantz
Mar 17, 2023
in HABARI, MICHEZO
0
MWENYEKITI WA CHAMA CHA  MABENKI TANZANIA (TBA) AONGOZA MAADHIMISHO  SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SEKTA YA MABENKI.
0
SHARES
156
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Bw. Theobald Sabi akitoa hotuba kwa washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake kutoka sekta za kibenki katika hafla iliyofanyika jana katika hoteli ya Onomo Jijini Dar es salaam.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA), Bi. Tusekelege Joune akitoa hotuba  ya ufunguzi katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa liyofanyika katika hoteli ya Onomo jijini Dar es Salaam

 

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Bw. Theobald Sab akisaliamiana na Mkurungezi wa Benki ya Equity Tanzania Bi Isabela Maganga katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika hoteli ya Onomo jijini Dar es Salaam jana.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Bw. Theobald Sabi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika sekta za kibenki iliyofanyika katika Hotel ya Onomo Jijini Dar es salaam.

 

Mkuu Kitengo cha Mauzo ya Fedha za Kigeni Wateja Wakubwa na Mashirika wa Benki ya NBC, Juliana Mwapachu akitoa mada katika majadiliano yaliyofanyika katika katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika hoteli ya Onomo jijini Dar es Salaam jana.

 

 

Dar es Salaam, Machi 16, 2023: Chama cha  Mabenki Tanzania (TBA)  kimeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa kila Machi 8 kwa kusisitiza kuwa ni muhimu kwa taasisi zote za kifedha nchini kuhakikisha kuwa makundi yote kwenye jamii hususani wanawake ushirikishwaji wao unapewa kipaumbele.

 

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika hoteli ya Onomo  jijini Dar es Salaam mapema leo, Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya Taifa (NBC) Bw. Theobald Sabi alisema ni muhimu sana kwa taasisi za kifedha kuhakikisha kunakuwa na ushirikishwaji mkubwa wa wanawake kwenye huduma za kibenki au kifedha nchini.  

“Tunatambua kuwa wanawake ni sehemu kubwa ya jamii yetu, zaidi ya asilimia 51 ya watanzania wote ni wanawake na kwa hivyo ni muhimu sana tunapoongeza ujumuishwaji wa kifedha kwenye jamii kundi la wanawake lisiachwe nyuma”. Alisema Sabi.

Bw. Sabi alibainisha kuwa kwa upande wa benki ya NBC wameanza na wafanyakazi wakijaribu kuhakikisha kuwa kama benki wanakuwa na sera rafiki kwa wanawake ili waweze kufikia malengo yao ya kikazi, kiajira, na kiuchumi.

Aidha naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA), Bi. Tusekelege Joune alisema kuwa inatia hamasa kuona kuwa benki nyingi nchini zimekuwa mstari wa mbele kubuni bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa maalum katika kukidhi mahitaji ya wanawake nchini.

“Tunashukuru kuwa benki zimekuwa mstari wa mbele katika kuja na bidhaa mbali mbali ambazo zimekuwa mahsusi kwa ajili ya wanawake hapa Tanzania. iwe mwanamke mfanyabiashara, mwanamke mtanzania, mwanamke ambaye kwa namna moja au nyingine akihitaji huduma za kibenki anakutana na bidhaa ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake,” alisema Bi. Joune.

Bi Joune aliongeza kuwa maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani kwa upande wa sekta ya kibenki kumekua na ongezeko kwa  benki kuja na huduma ya dhamana maalum kwa ajili ya wanawake. Kutolewa kwa hati fungani kwa ajili ya maendeleo ya wanawake n.k ikiwa ni jitihada mbali mbali zinzofanywa na sekta hio katika kuinua jinsia ya kike.

Mwisho______________

ADVERTISEMENT

 

 

 

 

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Tuliishi maisha ya shida sana kisa uchawi wa jirani!
HABARI

Tuliishi maisha ya shida sana kisa uchawi wa jirani!

by I am Krantz
Nov 30, 2023
EACOP Yakamilisha Utaratibu Wa Fidia Kwa Kukabidhi Nyumba Ya 339 Mkoani Tanga
HABARI

EACOP Yakamilisha Utaratibu Wa Fidia Kwa Kukabidhi Nyumba Ya 339 Mkoani Tanga

by I am Krantz
Nov 29, 2023
MAWAKALA WA USAJILI WA VODACOM TANZANIA WATEMBELEA AFRIKA YA KUSINI KUTOKANA NA UTENDAJI BORA WA KAZI.
HABARI

MAWAKALA WA USAJILI WA VODACOM TANZANIA WATEMBELEA AFRIKA YA KUSINI KUTOKANA NA UTENDAJI BORA WA KAZI.

by I am Krantz
Nov 29, 2023
NMB, Oryx Tanzania wazindua ‘Moto Mkali Bei Poa,’ kukopesha gesi ya kupikia
HABARI

NMB, Oryx Tanzania wazindua ‘Moto Mkali Bei Poa,’ kukopesha gesi ya kupikia

by I am Krantz
Nov 27, 2023
Kampeni Ya Serengeti Maokoto Ndani Ya Kizibo Yazidi Kusambaza Furaha Kwa Watanzania
HABARI

Kampeni Ya Serengeti Maokoto Ndani Ya Kizibo Yazidi Kusambaza Furaha Kwa Watanzania

by I am Krantz
Nov 27, 2023
NMB Mlipa Kodi Mkubwa na Bora Zaidi Tanzania 2023 🇹🇿
HABARI

NMB Mlipa Kodi Mkubwa na Bora Zaidi Tanzania 2023 🇹🇿

by I am Krantz
Nov 27, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TWEETS

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
March 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In