Mwigizaji maarufu katika filamu za The Wire na John Wick, Lance Reddick amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 60.
–
Nyota huyo ambaye pia alikuwa mwanamuziki alifariki kifo cha asili mapema Ijumaa nyumbani kwake jijini Los Angeles nchini Marekani.
–
Katika siku za karibuni alikuwa katika ziara za kuitambulisha filamu ya nne ya John Wick ambayo inatarajiwa kutoka Machi 24 mwaka huu akiwa mmoja wa waigizaji walioshiriki.
–
Tamthilia ya The Wire iliyoruka kuanzia mwaka 2002 hadi 2008 ilimtambulisha katika ulimwengu wa filamu, tasnia aliyoitumikia kwa miaka 25. Reddick ameacha mke mmoja na watoto wawili.