ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, June 5, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Naibu Waziri aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya michezo

I am Krantz by I am Krantz
Mar 27, 2023
in HABARI, MICHEZO
0
Naibu Waziri   aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya  michezo
0
SHARES
48
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa benki ya NBC, James Meitaron (wa pili kulia) wakimkabidhi kombe mshindi wa kwanza wa mashindano ya NBC Lugalo Open 2023 Ally Mcharo kutoka klabu ya TPC, Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi vya Gofu Lugalo, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo, Brigedia Generali mstaafu Michael Luwongo na Rais wa TLGU, Queen Siraki
Mwenyekiti Wa Klabu ya Lugalo Gofu Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo (katikati),Katibu wa Klabu hiyo, Luteni Kanali Shabani Kitogo(Kulia)na Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Alina Maria Kimaryo (wapili kushoto) wakikabidhi zawadi ya baiskeli kwa mshindi wa kwanza upande wa watoto (Juniors) katika Shindano la “NBC Lugalo Open 2023” , Omari Shabani. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Mashindano wa Chama Cha Mchezo wa Gofu Tanzania TGU, Ernest Sengeu.
NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma akicheza mchezo wa Gofu katika kufunga mashindano ya NBC Lugalo Open 2023 katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi vya Gofu Lugalo, Dar es Salaam  mwishoni wa wiki iliyopita wanaoshuhudia ni kulia ni Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa benki ya NBC, James Meitaron na kulia ni Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo, Brigedia Generali mstaafu Michael Luwongo .

           

Dar es Salaam, Tanzania: Machi 27, 2023 – Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma ameipongeza Benki ya NBC kutokana na jitihada zake za kusaidia maendeleo ya michezo mbali mbali nchini.

RelatedPosts

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA

Jun 5, 2023

SIMBA SC IMEWAHI KUCHEZA FAINALI CAF 1993

Jun 5, 2023

MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA

Jun 5, 2023
Load More

Akizungumza wakati  hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mchezo wa gofu wa NBC Lugalo Open 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi Lugalo jana, Mh. Mwinyijuma alisema benki ya NBC imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika sekta michezo hapa nchini na kuongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa benki hiyo.

“Nikiwa kama Naibu Waziri mwenye dhamana ya Utamaduni, Sanaa, na Michezo napenda kuishukuru benki ya NBC kwa kutuunga mkono katika jitihada za kuendeleza na kukuza maendeleo ya michezo.

ADVERTISEMENT

NBC imekuwa ikifadhili michezo mbali mbali kiwa ni pamoja na ligi ya Kuu ya Tanzania bara, Dodoma Marathon n.k. Ligi yetu kwa sasa ni moja ya ligi zinazotajwa kuwa ni ligi  bora barani Afrika na hii imewezekana kutokana  na mchango wabenki ya NBC,” alisema Mhe. Mwinjuma.  

Aliongeza: “Ni rai yangu kwa NBC kuendeleza kuweka mkono kwenye michezo yetu na kwenye sehemu nyingine za kijamii hapa nchini. Makampuni na taasisi nyingine pia ziige wanachokifanya benki ya NBC ili tuweze kupiga hatua kubwa na kwa haraka zaidi,”

Naibu Waziri aliipongeza NBC kufadhili michezo mbali mbali “Sikutegemea kuwakuta kwenye gofu, nimefurahishwa na jitihada zenu kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuimarisha michezo Tanzania. Hongereni sana NBC nyinyi ni mfano wa kuigwa,” aliongeza Mhe. Mwinjuma.

Aidha, Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa benki hiyo Bw. James Meitaron alisema kuwa kupitia sera ya kurudisha kwa jamii, benki hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali kuendeleza na kukuza michezo mbali mbali nchini.

“Tunaamini kuwa ushiriki wetu kwenye eneo hili la michezo pamoja na kusaidia juhudi za serikali katka maeneneo mengine, utasaidia kuboresha maisha ya Wanzania ikiwa pia ni sehemu yetu ya kurudisha kwa jamii .

Kama tulivyoahidi hapo awali, leo tumetoa tuzo mbali mbali kwa washiriki wa mashindano haya ya wazi ya NBC Lugalo 2023 yaliyoanza jana,” alisema Bw. Meitaron.

Kwa upande, mshindi wa kwanza wa mashindano hayo  Bw. Ally Mcharo aliishukuru benki ya NBC kwa kudhamini na kufanikisha mashindano  na pia aliushukuru uongozi wa Klabu ya Gofu ya Lugalo kwa kukubali kufanya mashindano hayo na kuwapa fursa vijana kuweza kuonyesha vipaji vyao.

ADVERTISEMENT

 

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA
HABARI

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
SIMBA SC IMEWAHI KUCHEZA FAINALI CAF 1993
MICHEZO

SIMBA SC IMEWAHI KUCHEZA FAINALI CAF 1993

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA
HABARI

MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
DIAMOND AWEKA KUFURU HII KWA DJIGUI DIARRA
MICHEZO

DIAMOND AWEKA KUFURU HII KWA DJIGUI DIARRA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
KUNANI MAGAZETINI LEO JUMANNE TAREHE 22 JUNI
HABARI

KURASA ZA MAGAZETINI LEO JUMATATU TAREHE 05 JUNI 2023

by I am Krantz
Jun 5, 2023
UJUE MPANGO MPYA WA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME NCHINI
HABARI

UJUE MPANGO MPYA WA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Jun 4, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In