Nyota wa Paris Saint Germain Neymar, inaonekana alipoteza Euro milioni 1 inayojadiliwa kuzidi bilioni 2 za Tanzania akicheza kamari mtandaoni siku ya Alhamisi.
–
Kulingana na ripoti kutoka duka la Globo Esporte la Brazil, alipoteza euro milioni 1 ndani ya saa moja tu, na waliomshuhudia akipoteza mchezo wake walidiriki kusema alionekana akilia na kupiga yowe kwa uongo na alirekodiwa akiwa mubashara (live) kwenye baadhi ya majukwaa ya mtandaoni.
–
Inaripotiwa kuwa tukio hilo lilirushwa kwenye chaneli yake ya Twitch. Nyota huyo wa Paris Saint Germain ambaye hupokea mabilioni ya pesa kwa mwezi, ameachwa ajipange na kujitazamia afya yake baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda uliosalia kwenye msimu huu kutokana na jeraha la kifundo cha mguu.