ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Sunday, April 2, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

ODINGA AZINDUA MAASI DHIDI YA RUTO

Kenya

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Mar 10, 2023
in HABARI
0
ODINGA AZINDUA MAASI DHIDI YA RUTO
0
SHARES
28
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

MAANDAMANO KENYA YAHISIWA KUWA MAKUSUDI

MAANDAMANO KENYA YAHISIWA KUWA MAKUSUDI

Mar 31, 2023

UKAME WAUA VIUMBE HAI KENYA

Nov 17, 2022

Air Tanzania yaitakia Kenya Uchaguzi wa Amani

Aug 10, 2022
Load More
ADVERTISEMENT
Legal hurdles to block Ruto, Raila's State House race - The InformerKiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Bw Raila Odinga jana alizindua rasmi uasi kamili dhidi ya serikali ya Rais William Ruto baada ya siku 14 aliyoipa kukamilika Jumatano usiku.
Waziri Mkuu huyo wa zamani aliongoza vinara wenzake Kalonzo Musyoka, Martha Karua na Eugene Wamalwa katika muungano huo wa upinzani kutangazia wafuasi wake sababu za kuasi serikali anayosisitiza sio halali na akawasilisha salamu za Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa wafuasi wake.
“Leo (jana Alhamisi) tunatimiza ahadi yetu kwa Ruto na serikali yake isiyo halali ya Kenya Kwanza. Tunaachilia nguvu za watu zifanye kazi na kuzindua vuguvugu la Movement For Multi Party Democracy,” Bw Odinga alisema huku akihimiza wafuasi wa Azimio kuasi, kugomea na kuandamana dhidi ya serikali ya Rais Ruto.

Uasi wa Azimio pia unatokana na kile ambacho Odinga alidai ni “ushuru uliovuka mipaka ambao Wakenya wanatozwa na serikali unaoua biashara, kufanya familia kuwa masikini na kuharibu nafasi za uwekezaji”.

“Utozwaji wa ushuru huu ni lazima ukome ili uchumi wa Kenya uweze kufufuka kwa sababu hii, lazima serikali ya Ruto iondoke mamlakani,” alisema.

Katika uasi huo ambao Bw Odinga aliashiria utafikia kilele Machi 20, 2023, Azimio italalamikia uagizaji wa chakula kilichobadilishwa kisayansi (GMO) ambao alisema ni mpango wa kuharibu uchumi wa eneo linalokuza chakula nchini na kufanya Wakenya kuwa watumwa wa kampuni kubwa za Amerika.

Aidha, uasi huo utalenga kusitishwa kwa mchakato wa kuajiri makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ulioanzishwa na Rais Ruto huku Bw Odinga akisisitiza kiongozi wa nchi anajipanga kuiba uchaguzi mkuu wa 2027.

Alipotoa makataa ya siku 14 kwa Rais Ruto mnamo Februari 22, Bw Odinga alitaka sava ambazo IEBC ilitumia katika uchaguzi mkuu wa 2022 kufunguliwa ili kubaini ukweli wa aliyeshinda, takwa ambalo Rais Ruto alikataa kutimiza.

Bw Odinga sasa anahimiza wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uasi na maandamano akisema ana hakika Rais Ruto alishirikiana na aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC kumpokonya ushindi.

“Kwa kuiba kura na kupindua ushindi wa watu na kukataa kufungua sava kujua ukweli, ni lazima Ruto aende,” alisema.

Uasi huo, akaeleza Bw Odinga, pia unatokana na kunyanyashwa kwa makamishna wanne wa IEBC Juliana Cherera, Irene Marsit, Justus Nyang’aya na Francis Wanderi kwa kukataa matokeo yaliyoonyesha kwamba, William Ruto alishinda urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Azimio pia inalaumu Rais Ruto kwa ‘kuteka na kudhibiti’ Mahakama na Bunge na kunyima asasi za serikali uhuru zinazopatiwa na katiba, kupalilia ukabila katika uteuzi wa nyadhifa kuu serikalini na kubuni ofisi kinyume cha katiba ili kuwazawadi wandani wake na familia zao na kugawanya nchi kwa misingi ya kidini.

Azimio ilifufua madai iliyotumia wakati wa uchaguzi mkuu ya unyakuzi wa mashamba na kutoweka kwa mashahidi wa kesi iliyomkabili Ruto katika Mahakama ya Kimataifa kuhusu uhalifu (ICC) kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2008.

Walilaumu Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kudai serikali ya Kenya ni kampuni na wenyehisa ni walioipigia kura.

“Tunaanza kwa kuambia Ruto na Gachagua kwamba, sisi ndio wenyehisa wa kweli kwa nchi hii, watu wote wa Kenya ni wenyehisa wa nchi yetu na hatuwezi kuvumilia serikali haramu.

Akaendelea: “Ni wakati wa vitendo, tujitokeze wote, popote tulipo ili sauti zetu zisikike na kuheshimiwa na baada ya kufanya tutakachofanya kokote katika kila kona ya nchi, tutakusanyika Nairobi kwa maandamano makubwa Machi 20 2023,” akatangaza Bw Odinga ambaye aliwasilisha salamu kutoka Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Bw Raila Odinga jana alizindua rasmi uasi kamili dhidi ya serikali ya Rais William Ruto baada ya siku 14 aliyoipa kukamilika Jumatano usiku.

Related

Tags: Kenya
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

EX MSUMBUFU KUFUNGWA JELA MIAKA MITANO
HABARI

EX MSUMBUFU KUFUNGWA JELA MIAKA MITANO

by Shabani Rapwi
Apr 2, 2023
CAMERA ILIYOPOTEA MIAKA 13 YAPATIKANA KWENYE MATOPE PICHA BADO ZIPO VIZURI

AFUKUA MAITI YA MAMA YAKE NA KUKAA NAYO NDANI

MUUGUZI AFARIKI AKIJIFANYIA HUDUMA MWENYEWE

CHINA NA BRAZIL ZAIKATAA DOLA YA MAREKANI

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

Apr 1, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In