Wachezaji wawili wa mpira wa miguu nchini Kenya wamefariki dunia siku Jumamosi Machi 11, baada ya kupigwa na radi wakati mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Manyansi FC dhidi ya Gianchore FC katika Uwanja wa Manyasi uliopo Kaunti ya Kisii nchini humo.
–
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Kaskazini la Kitutu Chache, Evans Akanga alisema wachezaji hao walipigwa radi na kufariki papo hapo wakati wa mchezo huo wa kirafiki ukiendelea.
–
Wachezaji wengine wawili walinusurika kifo na duru zinasema wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Nyamira ambapo walipelekwa kwa ajili ya huduma ya kwanza.