Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China Xi Jinping kwa kuchaguliwa tena kuliongoza Taifa hio kwa muhula mwingine baada ya kumaliza muhula uliopita.
Rais huyo wa China alichaguliwa bila Pingamizi kutokana na weledi na jitihada alizozionyesha katika msimu ulioisha wa uongozi wake katika nafasi hio.
Aidha Rais Samia amesisitidha kwa kutegemea muendelezo wa ushirikiano zaidi kwa mataifa hayo mawili kama ilivyo kuwa hapo awali.
“Pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais Xi Jinping kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China. Natarajia kuendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa ushirika kati ya Tanzania na China.”