Dj na muigizaji Romy Jons maarufu RJ The Dj ameibuka baada ya vifo vya mastaa wa mziki Africa, AKA na Costa Titch akisema vifo hivyo vilivyoongozana vinaleta msongo wa mawazo mitaani.
–
Romy Jons ameshea ujumbe huo mzito akiandika “Hivi vifo vya ndugu zetu,marafiki zetu vilivyoongozana kwa pamoja vimezidi kuongeza depressions kwa kiasi kikubwa sana mtaani. Ukichangia ugumu wa maisha na nafsi ya kuwaza kifo na kutokua na amani ya nafsi kuongezeka zaidi.
–
Cha kushauri kwa sasa ni kushkuru na kumuomba muumba wa kila kitu akujaalie nafsi yenye utulivu na mwisho mwema. Unapowaza kifo kwa muda mrefu basi jua wewe ni binadamu uliekamilika na hakuna tatizo lolote hapo”.