Kutoka kwa Romyjons maarufu zaidi Rj The Dj, kaka wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameomba Radhi kwa Mashabiki zake, Wafanyabiashara Wenzake na watu wote kwa Ujumla kwamba hatoweza kuchukua Show yoyote ile kwa sasa mpaka pale atakapomaliza mfungo
–
Kupitia Ukurasa wa Instagram #RjTheDj amethibitisha hilo kwa kuandika
–
“NIOMBE RADHI PIA KWA WAFANYABIASHARA WENZANGU NA MASHABIKI ZANGU KWA UJUMLA KWAMBA SITOWEZA TENA KUCHUKUA SHOW “EVENTS” MPAKA HAPO TUTAKAPOMALIZA MFUNGO IN SHA ALLAH
–
KWA KUMALIZIA NIWAOMBE MASHABIKI,MARAFIKI ZANGU HASA WA KIKE TUSITUME SANA MESSEGE ZISIZO NA TIJA “UMUHIMU”IN SHA ALLAH
–
YA ALLAH TUNAKUOMBA UTUFIKISHE SALAMA KWENYE MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI NA UENDE UKAPOKEE TOBA ZETU
–
KWA PAMOJA TUSEME AMIN IN SHA ALLAH
TAFADHALI” – Amefunguka Romy Jons.