Mamlaka ya serikali ya Jiji la Berlin nchini Ujerumani imeruhusu kuanzia sasa taratibu zibadilishwe ili wanawake waruhusiwe kuogelea vifua wazi katika swimming pools za umma (public) kama ilivyo kwa wanaume katika jiji hilo ili kuleta usawa wa kijinsia bila ubaguzi
–
Hii imekuja baada ya mwanamke mmoja kupeleka malalamiko yake akieleza kukataliwa kuogelea kifua wazi kinyume na matakwa yake ilihali wanaume wanaruhusuiwa bila bughudha Yeyote
–
Malalamiko yake yametiliwa maanani baada ya uchunguzi kufanyika, Kabla ya marekebisho yanayotarajiwa, wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuongelea vifua wazi kama wanaume katika swimming pools zisizo za binafsi na mwanamke akibainika kaogelea kifua wazi anaambiwa avae sidiria,swimming costume au ataondolewa sehemu husika