ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Sunday, April 2, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

SIMBA SC YAMUAHIDI MAKUBWA RAIS SAMIA, DHIDI YA HOROYA

Dar es Salaam

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Mar 13, 2023
in MICHEZO
0
SIMBA SC YAMUAHIDI MAKUBWA RAIS SAMIA, DHIDI YA HOROYA
0
SHARES
25
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

May be an image of 1 personBaada ya Timu ya Simba kuibuka na  ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, uongozi wa klabu hiyo umesema ni jambo zuri kuwa na Rais wa nchi anayependa michezo kiasi cha kuongeza motisha katika utafutaji magoli muhimu ya kuzivusha timu za nchi yake kwenye michuano ya Kimataifa.

Hayo yamekuja kutokana na ofa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa Sh Milioni 5 kila goli litakalopatikana kwa timu za Simba na Yanga, Simba ikishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati mtani wao wa jadi Yanga, akicheza Kombe la Shirikisho.

RelatedPosts

BACCA’ HAKUAMINI ATAJWA KUANZA DHIDI YA US MONASTIR

BACCA’ HAKUAMINI ATAJWA KUANZA DHIDI YA US MONASTIR

Mar 23, 2023

CHAMA AINGIA 10 BORA AFRIKA

Mar 22, 2023

SIMBA YAWEKA HISTORIA MPYA KLABU BINGWA AFRIKA

Mar 22, 2023
Load More

Akizungumza jijini Dar es Salaam Msemaji wa Simba, Ahmed Ally, alisema si tu Rais Samia anatamani timu za Tanzania zifanye vizuri Kimataifa, bali pia anashiriki kikamilifu katika mbinu ya utafutaji wa magoli muhimu ya kuzisaidia timu za nchi yake.

Alisema hali hii inaongeza chachu ya wachezaji, mashabiki, wanachama na viongozi wote kuona wana deni kubwa kwa rais wao, hivyo kuongeza bidi kubwa kushinda kwenye mechi zao.

ADVERTISEMENT

“Si tu Rais Samia anataka twende mbele, bali pia anaingia kwenye watafutaji wa magoli, kwa maana kununua goli katika mechi ngumu kama hizi, anamaanisha anataka wachezaji wacheze jihadi ili kuyapata kwa lengo moja tu timu ishinde na kupata pointi muhimu.

“Mambo kama haya kufanywa na mtu mkubwa kama Rais wa nchi yanatia moyo, ukizingatia anayefanya haya si mtu wa kawaida isipokuwa raia namba moja kwenye Taifa letu, hivyo sisi Simba tunamuahidi makubwa mama yetu kwenye mechi yetu dhidi ya Horoya Jumamosi ijayo kwa lengo moja la kufuzu robo fainali,” Alisema Ally.

Katika michuano ya Kimataifa inayoshirikisha timu za Simba na Yanga, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amejitokeza kununua kila goli litakalopatikana kwa Sh Milioni 5, ambapo mpaka sasa Yanga wamevuna milioni Milioni 30 kwa kufunga bao 6, huku Simba wao wakipata Sh Milioni 10 kwa kufunga mabao 2.

ADVERTISEMENT

Related

Tags: TOTAL CAF CHAMPIONS LEAGUE
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

SAKA AIBUKA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI EPL
MICHEZO

SAKA AIBUKA MCHEZAJI BORA WA MWEZI MACHI EPL

by ALFRED MTEWELE
Mar 31, 2023
HAWA HAPA NYOTA WANAOTAZAMWA ZAIDI KUTUA MAN ‘U’
MICHEZO

HAWA HAPA NYOTA WANAOTAZAMWA ZAIDI KUTUA MAN ‘U’

by ALFRED MTEWELE
Mar 31, 2023
CHELSEA YATAKA PAUNI MIL. 70 MAUZO YA MOUNT
MICHEZO

CHELSEA YATAKA PAUNI MIL. 70 MAUZO YA MOUNT

by ALFRED MTEWELE
Mar 31, 2023
TAIFA STARS YAAHIDI KUENDELEZA ILIPOISHIA
MICHEZO

TAIFA STARS YAAHIDI KUENDELEZA ILIPOISHIA

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
Naibu Waziri   aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya  michezo
HABARI

Naibu Waziri aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya michezo

by I am Krantz
Mar 27, 2023
NAIBU WAZIRI “FA” AIUNGA MKONO TAIFA STARS, AFCON 2023
MICHEZO

NAIBU WAZIRI “FA” AIUNGA MKONO TAIFA STARS, AFCON 2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2023
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In