Mitandao ya kijamii imeibuka kwa kasi nchini Tanzania na imechukua sura mpya kwa watu tofauti ambapo wapo wanaoichukulia kama fulsa ya kujipatia kipato kwa kuuza na kuzitangaza kazi zao, wapo wanaoitumia kama sehemu ya starehe kutuliza mawazo yao lakini pia imekuwa ni darasa huru kwa kila Mtanzania kwani kwa kuzingatia sheria tu unaweza kufanya chochote isipokuwa usivuke mipaka.
–
Hakika Ruben kutoka Iringa ni miongoni mwa wachekeshaji ambao walianza vizuri na mpaka sasa wanafanya vizuri, kutokana na aina yake ya uchekeshaji amejikuta anakuwa kivutio kwa watu wengi na kujipatia mashabiki rukuki, ambapo kwenye mtandao wake wa Instagram bado kidogo akifikishe wafwasi milioni moja, hii inaonyesha ni kwa kiasi gani jamii inamkubali.
–
Lakini tangu wiki hii ianze kumekuwa na video inayosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Hakika akiwa live na wenzake kwenye mtandao wa TikTok ambapo kuna maneno yasiyo na hekima alikuwa anayaongea, kwenye maneno hayo alikuwa anajitambulisha kama mshiriki wa mapenzi ya jinsia moja kwa kumgombania mwanaume mwenzao yeye na mwenzake.
–
Kutokana na CV ya Hakika na heshima kubwa aliyoitengeneza Watanzania wengi wameonyesha kuchukizwa na kitendo hicho cha kishetani huku wengi wakimtukana na kumtaka arejee kwa Mungu wake aombe msamaha.
–
Yote tisa, kumi mjadala huo umefika hadi nchini Kenya ambapo baadhi ya Wanahabari wameonyesha kukemea kitendo hicho na kuwaasa wazazi kuwaweka mbali watoto wao na mtandao wa Tiktok kwani si salama kwa watoto maana umekuwa kama uwanja wa kuhamasisha na kujifunza ngono.
–
Hata hivyo licha ya kuitwa Polisi, Hakika mwenyewe ameonyesha kutokujali kwani licha ya watu kumuomba abadirike bado ameendelea kuposti video za kujitangaza zaidi kuwa ni muhusika wa mambo hayo huku akifunga sehemu ya komenti kuwazuia watu wasiandike chochote.
–
Chanzo : Mtandao