Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema licha ya historia nzuri ya mkoa wa Tabora na mchango wake katika pato la taifa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitano masikini zaidi nchini Tanzania.
–
Zitto amesema kwa miaka mitano tumbaku ya mkoa wa Tabora pekee imeliingizia taifa fedha za kigeni shilingi milioni 848 lakini maisha ya wananchi wa Tabora hayafanani na ukweli huo.
ADVERTISEMENT
–
Zitto amesema kama serikali itakua na dhamira njema inapaswa iwekeze kwenye kilimo na mnyororo wa thamani wa kilimo. Amesema hayo katika mkutano wa hadhara mkoani Tabora.