Timu ya taifa ya Tanzania @taifastars_hii leo inatarajiwa kwenda kuanzia pale ilipoishia mwaka 2019 kwenye dimba la Mkapa, ambapo hii ilikuwa ni mara ya mwisho kwa timu hizi mbili kukutana kwenye kwenye dimba la Mkapa katika mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON.
Hivyo hii leo kwa mara nyingine tena timu hizi mbili zinakutana kwenye michuano ileile ya AFCON katika dimba la Mkapa huku Taifa Stars wakiwa wameshinda mchezo wa kwanza kwa goli 1-0, mchezo uliochezwa huko nchini Misri Machi 24, 2023.
Aidha Taifa Stars waliichapa Uganda The Cranes mabao 3-0, mabao yaliyofungwa na nyota Mbwana Samatta, Erasto Nyoni pamoja na Aggrey Morris.
