Meneja wa Tanzania commercial Bank (TCB), Tawi la Musoma Hagai Gilbert (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa mabati 135 yaliyotolewa na Benki hiyo kwa Diwani wa kata ya Kinyari, Mh Mkingi Itagata kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyamkoma wilayani Butiama.
Maofisa wa Tanzania Commercial Bank wakiongozwa na Meneja Benki
hiyo tawi la Musoma Hagai Gilbert pamoja na uongozi wa kijiji cha Nyamikoma
wakikagua ujenzi wa kituo cha Afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo
TCB imeguswana kuchangia kwa kutoa msaada wa mabati 135 kwa ajili ya kuendeleza
ujenzi huo
Wananchi
wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Butiama wakisaidia kushusha mabati 135 yaliyotolewa na
Tanzania Commercial Bank (TCB) kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa
zahanati.
Tanzania commercial
bank imekabidhi mabati 135 katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya
Butiama mkoani Mara kwa dhamira ya kuunga mkono juhudi za serikali katika
juhudi zake za kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya afya.
Msaada huo ulitolewa
leo katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butihama mkoani mara na
kupokelewa na Diwani wa kata ya kinyare Mh. Mkingi Itagata.
Pamoja ya kuishukuru
Benki ya TCB wakati akipokea msaada huo, Diwani wa kata ya Kinyare Mh Mkingi
Itagata amesema kuwa bado kuna uhitaji ili ujamilisha ujenzi wa kituo cha afya
kwani gharama ya ujenzi ni milioni 150 lakini hadi sasa kiasi walichokusanya ni
milioni 47.
“Serikali pamoja na
wazazi tutaongeza nguvu kwenye ujenzi huu maana wananchi wamekuwa
wakifuata huduma ya afya mbali kidogo na kijijini hapo.” Amesema Mkingi.
Akiongea baada ya
kukabidhi msaada huo, Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Musoma Gilbert Hagai
aliwasihi wananchi wa kijiji hicho kuwa TCB itaendelea kuunga mkono
juhudi za wananchi wapenda maendeleo na kuhakikisha kuwa benki hiyo inasogea
huduma zake karibu.
Aidha pia
amewapongeza wazazi na uongozi wa kijiji kwa jitihada zao za kuchangia na
kuanza ujenzi wa zahanati hiyo toka mwaka 2017 hii inaonesha kuwa ni kwa namna
gani kumekuwa na uhitaji.
“Benki yetu ya
Tanzania Commercial Bank ni mdau mkubwa wa Maendeleo, kwa kawaida kila
mwaka tunatenga fungu kutoka katika faida yetu kwa ajili ya kurudisha katika
jamii na tunaipa kipaumbele kwani Kuwekeza kwenye Elimu, Afya na maeneo
mbalimbali tukiwa kama benki tunaamini vitu hivi vyote vinatusiaida kupata wateja
na wafanyakazi wa benki yetu wa baadaye.
Tutaendelea
kuchangia na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais
wetu Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuboresha sekta ya afya kwa kadri
tunavyoweza na tunaahidi kwamba huu si mwisho.” Ameongeza gilbert.