Serikali ya Marekani inasema TikTok lazima iuzwe la sivyo ikabiliwe na uwezekano wa kupigwa marufuku nchini humo, kwa mujibu wa ripoti.
–
Programu (app) hiyo ya kushirikisha video, inayomilikiwa na kampuni ya Kichina ya ByteDance, inashutumiwa kwa kusababisha hatari ya usalam wa taifa kwa kukusanya data kutoka data za mamilioni ya watumiaji.
–
Ombi la kubadili umiliki, kwa mara ya kwanza liliripotiwa katika jarida la Wall Street Journal (WSJ), lilithibitishwa hilo.
–
Kampuni hiyo inasema mauzo ya kulazimishwa hayatabadili usambaaji wa data au upatikanaji wa programu ya TikTok.
–
Kwa miaka maafisa wa Marekani wamekuwa wakielezea hofu zai kwamba taarifa(data) kutoka kwa app hiyo maarufu zinaweza kuangukia mikononi mwa serikali ya Uchina.