Tetesi za usajili wa Kiungo wa Singida Big Stars, Bruno Gomes kuelekea Yanga Ss zimemuibua Afisa Habari na Mawasiliano wa Singida BS, Hussein Massanza ambapo amebainisha kuwa Hakuna Timu yoyote ambayo wamefanya nayo Mazungumzu juu ya kumuuza mchezaji huyo.
–
Massanza Akizungumza na Wasafi Media leo Machi 15, 2023 amesema kuwa Bruno hakusajiliwa kwaajili ya kushiriki Ligi Kuu pekee yake Bali kwa michuano ya kimataifa hivyo bado klabu hiyo haijaanza kumtumia ipasavyo katika malengo yaliyofanya wamsajili kiungo huyo.
–
“Tetesi tumezisikia lakini tunashangaa kwanini zitoke kipindi hiki? Sio Yanga tu, hakuna timu yoyote ambayo tumewahi kufanya nayo mazungumzo kuhusu kumuuza Bruno kwa sababu hatuna mpango huo, labda kama wanaongelea huko vibarazani.
–
“Jambo ambalo watu labda hawafahamu, Bruno hatukumsajili kwa malengo ya kucheza ligi kuu, tulimsajili kwa mipango mikubwa zaidi hasa michuano ya kimataifa. Kwahiyo hatujaanza hata kumtumia kwenye malengo yetu kama klabu.
–
“Hiki sio kipindi cha usajili kwahiyo binafsi nazichukulia kama propaganda tu kuelekea mechi yetu na Yanga hivi karibuni,” ameeleza Massanza.