Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha wafanyabiashara wa gesi nchini Tanzania Amos Jackson amewataka Watanzania wanaotumia gesi ya kupikia majumbani kuacha kununua gesi kwa msambazaji ama mfanyabiashara wa gesi ambaye hana mizani ya kupima ujazo wa gesi husika.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa wananchi wengi wao wamekuwa wakinunua gesi ambayo ujazo wake haujakamilika sambamba na kuwa na utamaduni wa kupima ujazo wa gesi kabla ya kununua na kuondoka nayo nyumbani.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT