Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amewataka vijana nchini kujitokeza na kuchangamkia fursa za kilimo.
–
Dkt. Mwinyi amesema hayo Ikulu, Dar es Salaam wakati wa mkutano wa maandalizi ya mkutano wa Afrika wa masuala ya Chakula na Kilimo (AGRF) unaotarajiwa kufanyia nchini mwezi Septemba mwaka huu.
–
Akitoa salamu za Zanzibar Dkt. Mwinyi amesema, kilimo ni sekta inayotoa ajira kwa Watanzania wengi, hivyo ni vema vijana wakachangamkia fursa hiyo.
–
Pia amesisitiza uwekezaji zaidi katika sekta ya kilimo hasa kwa kundi la Wanawake na Vijana.
–
Rais huyo wa Zanzibar amesema, Zanzibar ina hoteli zaidi ya mia sita zinazoweza kutumika kupokea Wawekezaji watakaofika nchini kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo.
–
“Kupitia sekta ya kilimo tutakapopata Wawekezaji kutoka nje, nasi Zanzibar tumeendelea kujipanga kwa kuwa na hoteli zaidi ya 600 ili kupokea Wawekezaji watakaokuja Tanzanai kuwekeza.” Amesisitiza Dkt Mwinyi