
Muswada huo una lengo la kuongeza umri wa kustaafu kutokea miaka 62 hadi 64.
Wanasiasa wa upinzani walipiga kelele,kuimba huku wengine wakizomea Bungeni wakati wale wanaomuunga mkono Rais Macron wakiimba mistari ya wimbo wa taifa la nchi hiyo kama mapokeo yao ya taarifa kuwa sheria hiyo inaweza ikapitishwa bila kupigiwa kura.
Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters,takribani raia 7,000 waliandamana jijini Paris kupinga mabadiliko hayo huku Polisi wakirusha mabomu ya machozi na kutumia mizinga ya maji ili kuwatawanya.
Waandamanaji hao walijibu mashambulizi hayo kwa kurusha mawe kwa maafisa wa usalama.
ADVERTISEMENT