Mbunge wa Viti Malaamu Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe Amewataka Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari Mtinko Kuongeza Jitihada katika Masomo yao na Kujiepusha na Mahusiano ya Mapenzi ili Kuepusha Athari Mbalimbali Zinazoweza Kusababisha Kutofikia Ndoto zao.
–
Akizungumza wakati Akikabidhi Taulo za Kike na Mpira kwa Ajili ya Michezo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Ulimwenguni Mhe. Mattembe Ametaja Athari hizo ambazo ni Kupata Mimba zisizotarajiwa,Maradhi,Kushindwa kuendelea na Masomo na Nyinginezo Nyingi.
Katika Hatua Nyingine Mbunge Huyo Amewahimiza Wazazi na Walezi Kuwaruhusu Watoto wa Kike Kushiriki katika Masomo ya Ziada ili kuwapa fursa kuongeza Uelewa katika Mada ambazo Zinawapa Changamoto Kuliko kuendelea Kuwazuia Kama Ilivyo kwa Hivi Sasa.
–
Wakizungumza Kando ya Maadhimisho hayo Baadhi ya Washiriki katika Maadhimisho hayo Wamemshukuru Mbunge Huyo kwa Kuwajali Huku Wakiiomba Serikali Kuwajengea Mabweni ili Kuwapunguzia Hatari Wanafunzi wa Kike Wanaotembea Umbali Mrefu Kufuata Shule.