
Mshindi wa droo ya “MastaBatakotekote”iliyokuwa ikiendeshwa na Benki ya NMb Ndugu,John Lubisha ameishukuru Benki hiyo kwa kuweka shindano hilo lililomuwezesha kuwa mshindi wa kwenda Dubai kwa mapumziko.
“Nilifurahi sana baada ya kupokea simu kwamba mimi nimekuwa mshindi, nashukuru Mungu kwa kupata hii nafasi,” amesema John Lubisha.
Aidha John ameongeza kwamba alikuwa anatumia kadi ya Nmb ya Mastercard (Kuchanja) kulipia bidhaa mbali mbali na hatimaye ameweza kupata ushindi katika droo hiyo.

“Ili kushiriki hizi droo mshiriki anatakiwa kuwa mvumilivu kwa kuendelea kutumia huduma ya kadi( kuchanja) kwa muda mrefu na siku moja anaweza kuwa yeye ndio mshindi,” amesema Lubisha
John amewashauri Watanzania kutumia kadi ya NMB Mastercard kwani ni rahisi lakini pia ni usalama zaidi kwani kutembea na pesa nyingi(Cash) si salama kwakuwa kuna matukio mengi ya kihalifu hata hivyo kutumia Mastercard kuna rahisisha maisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya kadi wa Benki hiyo Bw. Filbert Casmir amesema washindi hao wa kampeni ya “Mastabatakotekote” iliyoanzishwa mwezi wa kumi 2022 wamekabidhiwa tiketi zao tarehe 28 Februari 2023.
Washindi hao watalipiwa gharama zote watakazotumia Dubai ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio, hiyo yote ni kurudisha shukurani kwa wateja wa benki hiyo.
Aidha amewashauri Watanzania kuendelea kutumia Mastercard kwani benki hiyo itaendelea kuwa na kampeni mbali mbali zitakazoambatana na zawadi.

Benki ya NMB ilianzisha kampeni ya “Mastabatakotekote” ikiwa na malengo mbalimbali ya kuhamasisha wateja wao kutumia Mastercard, kuwajali wateja wao ambapo washindi waliopatikana wanaenda Dubai kwa mapumziko.