Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Askari wa Uhifadhi wanyama pori kanda ya kaskazini TAWA, wamekamata watu watatu wakazi wa kijiji cha Madunga wilayani Babati mkoani Manyara wakiwa na nyara za serikali meno sita ya Tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania millioni 100.
ADVERTISEMENT
–
ADVERTISEMENT
Kamanda wa Polisi Manyara ACP George Katabaz amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Frank John (26) Bashiru Ally (45) na Daniel Gabriel (39).