Mama mmoja mkazi wa Makambako aliyefahamika kwa jina la Fatma Kimbawala (80) amekutwa ameuwawa huku watoto wake wakihusishwa na mauaji hayo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na kuwepo kwa ugomvi wa kugombea mali za urithi.
–
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mama huyo alikuwa ni msimamizi wa mirathi hivyo watoto hao walikuwa wakitaka kugawana kitu ambacho kilipelekea kuwepo na mvutano katika ugawaji wa mali hizo.
–
“Huyo mama amekutwa amefariki lakini cha kushangaza wahisiwa wa kwanza ni watoto wake, hivyo jeshi la polisi tumewakamata watoto wake na tunaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hili”.
–
Aidha Kamanda Issa amewataka watu wote kufuata utaratibu katika masuala ya mirathi ikiwemo kutumia mahakama ama wazee wa kimila ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.