Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wanawake nchini kujiamini wakati wa kutekeleza majukumu yao.
–
Dkt. Mabula amesema hayo jana tarehe 8 Machi 2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Kwadeko wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
–
Amesema, wanawake wanatakiwa kufanya kazi zao huku wakielewa kuwa juu yao yupo mwanamke shujaa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.
–
“Kila mwanamke anayepewa nafasi akiwa mwenyekiti au kiongozi wa mahali fulani, anatakiwa kujiamini kwa kuwa wanawake wamemuweka pale” alisema Dkt Mabula.