Timu ya Wanawake ya Yanga, ‘Yanga Princess’ wakiwa wao ndiyo wenyeji wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya Wanawake ya Simba ‘Simba Queens’ katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
–
Simba Queens walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Jentrix Shikangwa dakika ya 30 mpaka wanakwenda mapumziko Simba Queens walikuwa mbele kwa bao 1-0.
–
Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi kwa timu zote mbili kushambuliana kwa zamu na mnamo wa dakika ya 77, Yanga Princess walisawazisha bao kupitia kwa Wogu Chioma.
–
Kwa matokeo hayo yanaifanya Simba Queens kukaa nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania wakiwa na alama 27, Yanga Princess wao wanakaa nafasi ya nne wakiwa na alama 22′.
–
Kinara wa Ligi hiyo ni Fountain Gate, ambao wapo kileleni wakiwa na alama 29, JKT Queens nafasi ya pili wakiwa na alama 28. Timu zote zilizopo nafasi ya kwanza mpaka ya nne zimeshacheza jumla ya mechi 12 mpaka sasa.