Kwa mujibu wa Mtandao wa FAR Post Klabu ya Yanga huenda ikakutana na rungu la FIFA la kufungiwa kusajili wachezaji kwa madirisha matatu mfululizo baada ya kushindwa kumlipa fidia kuvunja mkataba bila utaratibu kwa aliyewahi kuwa kocha wao Luc Eymael
–
Baada ya Eymael kushinda kesi Yanga ilielekezwa kumlipa fidia kocha huyo ya Dola za Marekani 152,000 sawa na Tsh Mil 355, Yanga ilipanga kumlipa kwa awamu tano kuanzia Oktoba 2022.
–
Yanga imelipa deni hilo kwa awamu mbili tu mwezi Oktoba na Novemba hivyo Yanga bado wanadaiwa Dola 99,000 pamoja na ada ya adhabu hiyo ambayo ni dola 5,000 na wamepewa hadi Machi 23, 2023.
–
Eymael amewahi kuzifundisha klabu kadhaa za Afrika kubwa Afrika zikiwemo Free State Stars na Polokwane City za Afrika Kusini, Al-Merrikh ya Sudan As Vita ya DRC.