Mchezaji wa mpira kutokea klabu ya PSG, Achraf Hakimi amewashangaza wengi akiwemo mkewe, baada ya kusajili mali zake zote kwa jina la Mama yake, hivyo kukosa umiliki halali wa mali.
–
Jambo hilo limegundulika baada ya mkewe, aliyefahamika kwa jina la Abouk, kudai talaka kutoka kwa mwanasoka huyo na kupeleka kesi huku akitaka mahakamani kusimamia ugawanyishwaji wa mali za Hakimi.
–
Hata hivyo, baada ya kufika mahakamani iligundulika kuwa mchezaji huyo anayelipwa kiasi cha zaidi ya Euro milioni moja za kimarekani kwa mwezi, sawa na zaidi ya Shilingi bilioni mbili za kitanzania, hana mali wala pesa yoyote kwani alizisajili kwa jina la Mama yake tangu alipokuwa na umri wa miaka 18.
–
Mpaka sasa Hakimi, ana miaka 31 na pindi akitaka kununua kitu chochote hutoa taarifa kwa Mama yake ambaye huwa akimnunulia vitu husimamia matumizi yake ya fedha.