Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Maryam Yahya Maulid mwenye miaka 25 leo, Aprili 14 saa 7:45 mchana amejifungua mtoto wa kiume akiwa ndani ya Boti ya MV Kilimanjaro V iliyokuwa ikitokea Zanzibar kwenda Dar es Salaam.
–
Mwanamke huyo amejifungua salama kwa msaada wa Daktari Suleiman wa Sealink na mtoto huyo amezaliwa na uzito wa kilogramu 2.5 na kupewa jina la Kilimanjaro V.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Mume wa mwanamke huyo, Isaka Musa amesema kwasasa mama na kichanga chake wanaendelea vizuri na wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Temeke kwaajili ya uchunguzi zaidi. Credit : Azam TV