Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Amani Martin maarufu kwa jina la Kasisi (47) mkazi wa Nzihi wilaya ya Iringa ambae pia ni kiongozi wa dini kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba kwa madai ya kudanganywa na shetani.
–
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi aliwaeleza wanahabari jana ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea Machi 28 majira ya saa saba mchana na kumsababishia maumivu makali sehemu za haja kubwa .
–
Alisema kuwa Kasisi ambae ni mkulima wa Kijiji cha Nzihi alidai kuwa alifanya tukio hilo baada ya kudanganywa na shetani na kuwa anajutia kutenda unyama huo kwa mwanae .
–
Alisema kuwa mama wa mtoto huyo Magreth Kaguo (29) ndie ambae alibaini mtoto wake huyo kulawitiwa na kuwa mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote.