Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa Baraka Ladslaus (kushoto) amesema wamekabidhi madawati 250 yenye thamani ya Sh. Mil 24.9 kwa shule tano za Mkengwa,Tacho,Nyamusi,Ngasaro,Nyihara zilizopo wilayani Rorya, kusaidia Serikali katika uboreshaji wa miundombinu ya Elimu na kurudisha kwa jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoka ameshiriki kukabidhi madawati 50 kati ya Madawati 250 ambayo yametolewa na Bank ya @NMBTanzania kwa shule Tano zilizopo wilayani humo kwa lengo la kusaidia kupunguza changamoto ya watoto kukaa chini na kuboresha ufaulu wao’
“Tuwashukuru@NMBTanzania sisi watu wa Rorya kutuwezesha kufikia lengo letu la mapambano ya kukabiliana na ufaulu mbovu, niwaombe walimu na Wanafunzi kutumia misaaada hii kama chachu ya kuongeza ufaulu wenu”Juma Chikoka Mkuu wa Wilaya ya Rorya.