ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 30, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

CRDB; DHAMANA YA MKOPO SI LAZIMA IWE NYUMBA

Dar es Salaam

MTEWELE ALFRED by MTEWELE ALFRED
Apr 27, 2023
in HABARI
0
CRDB; DHAMANA YA MKOPO SI LAZIMA IWE NYUMBA

Meneja Mwandamizi wa Biashara wa Benki ya CRDB, Agness Kisinini akizungumza katika kongamano la wajasiriamali wadogo na wakati lililoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) na limedhaminiwa na Ashton, Benki ya CRDB, Kampuni ya Usafirishaji DHL, Benki ya Stanbic, Benki ya NMB, Clouds Media na Ukumbi wa mikutano wa Dome.

0
SHARES
84
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

NBC yasaini Makubaliano na Serikali Kwaajili ya Kufadhili Masomo ya Ufundi kwa Wanafunzi 1,000

NBC yasaini Makubaliano na Serikali Kwaajili ya Kufadhili Masomo ya Ufundi kwa Wanafunzi 1,000

Jul 21, 2023

Benki ya Equity yaendelea Kujivunia Kutoa Huduma Bora kwa Gharama Nafuu Tanzania

Jul 14, 2023

HUDUMA YA NBC CONNECT YAFIKA MKOANI DODOMA

Jun 24, 2023
Load More

Meneja Mwandamizi wa Biashara wa Benki ya CRDB, Agness  Kisinini amesema dhamana ni suala mtambuka katika utoaji mikopo na si kwa wafanyabishara wadogo tu bali watu wote.

Amesema si lazima dhamana iwe nyumba jambo la msingi ni mkopaji kuzungumza na maofisa wa benki wanaoshughulika kwenye eneo hilo kuangalia kama anazo sifa za kukopesheka ikiwemo dhamana inatosha kufikia kiasi cha fedha anachotaka kuchukua.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Aprili 27, 2023 katika kongamano la Wafanyabiashara wachanga, wadogo na Kati (MSMEs), lililoandaliwa na Mwananchi Communications Limited na kukutanisha wadau ili kujadili nini kifanyike kuwawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi.

Amesema ugumu wa dhamana hutokana na msukumo wa wafanyabiashara wengi ambapo akili zao huwa katika kukuza biashara na wengine huwa na biashara zinazofanya vizuri lakini kwenye dhamana anakuwa hajaweka nguvu.

“CRDB tumelitambua hilo na kuangalia dhamana upande wa wanawake na wateja wa kawaida. Kwa upande wa wanawake tumekuja na Malkia akaunti ambayo itamsaidia mwanamke kufikia malengo yake” amesema.

Amesema akaunti hiyo humuwezesha mtu kuweka kidogokidogo na baada ya muda anafikia anachotaka na hiyo inamsaidia kutengeneza dhamana katika mfumo wa fedha taslimu.

Kisinini amesema dhamana si lazima iwe nyumba bali zipo za aina nyingi ikiwemo fedha inayoweza kumfanya mtu apate mikopo kwa haraka na riba ya chini kwa sababu tayari anayo fedha pesa inayopunguza hasara kwa benki.

“Mtu anapotoza riba anaangalia na hasara anayoweza kupata, kuwa huyu mtu asipofanya vizuri na asipolipa tukauza hii dhamana tutauza haraka au itatusumbua? Sasa kwa upande wa fedha haina hasara ndiyo maana riba yake inakuwa chini,” amesema Agness.

Amesema kwa upande wa CRDB, wateja wadogo ni wale ambao mzunguko wao kwa mwaka unaanzia Sh100,000 hadi Sh250 milioni.

“Katika utoaji mkopo huyu anaweza kupata hadi Sh50 milioni na zaidi ya mikopo wametengenezewa akaunti ambazo wakizitumia vizuri zinaweza kuwasaidia kupata mitaji kwa sababu wakiwa na nidhamu ya kuweka fedha baada ya muda anapata mtaji  na kufanya wanachotaka kupita akaunti ya hodari,” amesema Agness.

Amesema akaunti hiyo imeondoa makato yote isipokuwa ya kiserikali jambo linaloweza kuwafanya kuweka fedha hadi mwaka mmoja bila kukatwa.

“Inaweza kuwa kama kibubu kinachomsaidia kutunza fedha zake zisizokatwa na uhakika kwa sababu kama tupo kwenye kundi tunaweka mmoja mmoja mwenzangu anaweza kutumia ile fedha na kuna siku naihitaji nikaikosa lakini kwa kupitia akaunti hii nina uhakika na kile ninachokifanya,”amesema.

Kongamano hilo limedhaminiwa na Ashton, Benki ya CRDB, Kampuni ya Usafirishaji DHL, Benki ya Stanbic, Benki ya NMB, Clouds Media na Ukumbi wa mikutano wa Dome.

CC; Mwananchi

Related

Tags: CRDB BANKMKOPOUJASIRIAMALIWIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
MTEWELE ALFRED

MTEWELE ALFRED

Related Posts

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO
HABARI

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
TSO WAZINDUA GALA DINNER
HABARI

TSO WAZINDUA GALA DINNER

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
CHANJO YA MBWA NI MUHIMU
AFYA

CHANJO YA MBWA NI MUHIMU

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
52 WAFARIKI KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID NCHINI PAKISTAN
HABARI

52 WAFARIKI KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID NCHINI PAKISTAN

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
SEKTA YA MADINI YAJA NA MBT KAMA FURSA KWA VIJANA
HABARI

SEKTA YA MADINI YAJA NA MBT KAMA FURSA KWA VIJANA

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
TUNZAA YATANGAZA USHIRIKIANO MKUBWA NA KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA M-PESA 
HABARI

TUNZAA YATANGAZA USHIRIKIANO MKUBWA NA KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA M-PESA 

by I am Krantz
Sep 29, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

April 2023
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
« Mar   May »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In