Shirika la Afya Duniani (WHO), limetoa tahadhari kuhusu dawa ya Kikohozi “Guaifenesin TG SYRUP” ambayo imekutwa katika Visiwa vya Marshall na nchini Micronesia katika Bahari ya Pasifiki.
–
Dawa hiyo imetengenezwa na kampuni ya QP Pharmachem Ltd ya Punjab, India.
–
WHO imesema kuwa vipimo vya dawa hiyo vimeonyesha kiasi cha kemikali za diethylene glycol na ethylene glycol ambacho hakikubaliki. Kemikali hizo ni sumu kwa binadamu na zinaweza kusababisha kifo.
–
Tahadhari hii imekuja miezi kadhaa baada ya Shirika hilo kuhusisha dawa zingine za kikohozi zilizotengenezwa India na vifo vya watoto nchini Gambia na Uzbekistan.